Back to top

ASKARI WA JESHI WAWAPIGA ASKARI POLISI, KENYA

28 April 2024
Share

Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF), limesema linachunguza tukio la askari wa Jeshi hilo kuwashambulia kwa kipigo askari wa Jeshi la Polisi nchini humo, katika eneo la Kivuko cha Likoni, mjini Mombasa.
.
Hatua hiyo inafuata baada ya kusambaa kwa video iliyoonyesha Maafisa wa KDF wakizozana na Maafisa wa Polisi, mzozo ambao baadae ulionekana kwenda mbali zaidi baada ya Askari mmoja wa KDF kuonekana akimpiga Askari wa Jeshi la Polisi. 
.
Jeshi hilo limesema linafuatilia kisa hicho ambacho kimeleta sintofahamu kwenye jamii, huku likisisitiza kuwashughulikia Askari wake wote watakaokutwa na hatia. #citizentvKenya