Back to top

LINDI: JITIHADA ZA KUREJESHA MAWASILIANO ZINAFANYIKA

05 May 2024
Share

Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), umewataka wananchi na madereva wanaotumia Barabara ya Lindi – Dar es Salaam, ambayo imeharibiwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha, kuwa na subira kwani inaendelea kufanya kila linalowezekana kurejesha miundombinu ya barabara hiyo.
.
Hayo yamebainishwa na Meneja wa TANROADS, Mkoa wa Lindi, Mhandisi Emil Zengo, alipotembelea na kukagua uharibifu uliotokea katika eneo la Somanga - Mtama, ambalo leo, Mei 05, 2024, majira ya asubuhi maji yamefurika kwa wingi na kuharibu eneo la takribani mita 80 katika barabara hiyo, na kukata tuta katika eneo la Mikereng'ende umbali wa km 10 kutokea Somanga uelekeo wa Lindi.