Independent Television Ltd
Idara ya mipango miji yashauri serikali kutojenga wilaya kwenye misitu katika kijiji cha Katuma,Katavi.

Wakati serikali ikisisitiza dhamira yake ya kujenga makao makuu ya halmashauri ya wilaya kwenye misitu katika kijiji cha Katuma wilaya ya Mpanda mkoani Katavi, ofisi ya mipango miji kanda ya Tabora imesema eneo hilo halina sifa ya kuanzisha makazi na imeshauri kutafutwa kwa eneo jingine na kuiacha misitu hiyo iendelee kutumika kwa shughuli za uhifadhi. 

Meneja wa mipango miji na matumizi bora ya ardhi kanda ya Tabora inayohudumia mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi na mikoa ya kanda ya ziwa Peter Gambaloya amesema itashangaza kuona serikali inaanzisha makao makuu kwenye misitu wakati yenyewe inatakiwa kuwa mstari wa mbele kuihifadhi misitu hiyo kwani inaona umuhimu mkubwa kwa vyanzo vya maji na pia ni makazi ya wanyamapori na Sokwe ambao ni miongoni mwa viumbe adimu walio katika hatari ya kutoweka.
 
Nae mtaalam wa ikolojia kutoka hifadhi ya taifa ya Katavi Elisa Manase amesema misitu ya wilaya ya Mpanda imekuwa na mchango mkubwa kwa mtiririko wa maji ya mto Katuma ambao umekuwa ukikauka kila mwaka wakati wa kiangazi kutokana na uharibifu wa mazingira kwenye misitu hiyo na kwamba ujenzi wa makao makuu ya halmashauri katika kijiji cha Katuma utakuwa unapingana na juhudi za wadau kuimarisha uhifadhi endelevu wa misitu na vyanzo vya maji.
 
Utafiti unaoendelea kufanywa na mhadhiri mwandamizi wa kitivo cha maliasili, sayansi na saikolojia cha chuo kikuu cha Livepool cha nchini Uingereza Alexander Piel, umeonyesha kuendelea kupungua kwa kasi kwa idadi ya sokwe wa Tanzania ambao miaka ya nyuma walikuwa wengi lakini ongezeko la shughuli za binadamu kwenye milima ya wansisi na misitu mingine limeuweka rehani uhifadhi wa Sokwe wa Tanzania viumbe ambao hufanana kijenetiki na binadamu kwa zaidi ya asilimia 98.
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Kuelekea uchumi wa viwanda. Je mfumo wa elimu umebadilika kujibu mahitaji ya nchi
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather