Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) imeendelea na ufuatiliaji wa huduma zake kwa wateja kwa kutembelea wauzaji wa bidhaa zake, hususan chanjo za mifugo, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja inayoendelea kote nchini. Zoezi hilo linafanyika kwa lengo la kubaini namna huduma za TVLA zinavyowafikia wateja, kusikiliza maoni ya wadau wanaosambaza bidhaa hizo, pamoja na kujadili njia bora za kuimarisha ubora na upatikanaji wa huduma.