Independent Television Ltd
MCT wafungua kesi ya kupinga sheria ya huduma za vyombo kwenye mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ).

Baraza la habari Tanzania MCT kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki za binadaamu, wamefungua kesi ya kupinga sheria ya huduma za vyombo kwenye mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam  mara baada ya kufunguliwa kwa kesi hiyo, katibu mtendaji MCT, Kajubi Mukajanga amesema hatua hiyo inalenga kuipinga sheria hiyo ya huduma za habari.
 
Naye  mkurugenzi wa kituo cha LHRC, DkT. Hellen Kijo Bisimba  amesema wameamu kwenda katika mahakama hiyo wakiamni kuwa ipo kwa ajili ya watu wote na haina vizuizi vyovyote, kwani nchi ya Tanzania ipo Afrika Mashariki.
 
Kwa upande wake mratibu wa mtandao wa watetezi wa haki za binadamu Onesmo Olengurumwa amesema wamekuwa wakiwatetea wale waliokuwa mstari wa mbele hasa waandishi wa habari kwa kuwa ni watetezi wakubwa katika jamii.
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Kuelekea uchumi wa viwanda. Je mfumo wa elimu umebadilika kujibu mahitaji ya nchi
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather