Independent Television Ltd
Tanzania na Korea kushirikiana kuhifadhi na kuendeleza utalii nchini.

Tanzania na Korea zimekubaliana kushirikiana kuboresha uhifadhi na  kuimarisha miundombinu ya utalii na tayari serikali ya korea kupitia shirika lake la misaada la (KOICA) imetoa  dola milioni 1.5 sawa na zaidi ya bilioni 2 (mbili) kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kimataifa cha  kutolea taarifa za mienendo ya wanyamapori ambacho ni sehemu ya utekelezaji makubaliano hayo.

Akizungumza katika hafla ya kuweka  jiwe la msingi la ujenzi wa kituo hicho kinachojengwa Serengeti waziri wa maliasili na utalii Mh Prof Jumanne Maghembe na baadhi ya wadau wa utalii wamesema hatua  hiyo ni sehemu ya mikakati ya kuendelea kufungua milango ya kuvutia  watalii kutoka bara la Asia.

Kwa upande wake mwakilishi wa shirika la hilo la misaada la Korea (KOICA) Dr. Wooyong Chung, amesema nchi yake imedhamiria kikamilifu kusaidia jitihada za Tanzania za kuimarisha uhifadhi hasa katika maeneo ya urithi wa dunia ikiwemo hifadhi ya Serengeti.

Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Utaratibu wa viongozi kukutana na wananchi kusikiliza kero zao. Je, utasaidia kuongeza uwajibikaji kwa watendaji serikalini?
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather