Independent Television Ltd
Manispaa ya Kinondoni yatoa miezi sita kwa wauza nyama kuboresha mazingira kufanyia biashara hiyo.

Uongozi wa manispaa ya kinondoni jijini dar es salaam umetoa muda wa miezi sita kuhakikisha kila bucha linalouza nyama linakuwa na mashine vza kukatia nyama ikiwa ni pamoja na kuboresha mazingira yake ya kufanyia biashara hiyo.

ITV imetembelea mabucha mengi tu ndani ya manispaa ya Kinondoni na kukuta mengi kati yake yakitumia magogo katika kukatia nyama zake jambo ambalo ni hatari kwa walaji wa nyama hizo.
 
Manispaa inasema ni asilimia 60 pekee ya mabucha yote yanayotumia mashine huku ikitoa miezi sita kwa wafanyabiashara kuhakikisha wanaboresha miundombinu yao ndani ya mabucha.
 
Maafisa kutoka kampuni ya ranchi ya taifa wanasema ni muhimu kwa wafanyabiashara wa nyama kuiga kwao kwani mazingira bora ya uuzaji wa nyama pia ni sababu ya kumuepusha mlaji na magonjwa mbalimbali anayoweza kuyapata.
.
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Wakulima kulazimishwa kuuza korosho kinyume na bei elekezi. Je ni utawala bora?
Ndio
Hapana
Vote Now
Results
Weather