Independent Television Ltd
Wenyeviti wa serikali za mitaa nchi nzima watoa masaa 24 kwa katibu mkuu wa TAMISEMI kuwaomba radhi

Wenyeviti wa serikali za mitaa nchi nzima wametoa masaa 24 kwa katibu mkuu wa TAMISEMI kuwaomba radhi na kutengua agizo la kuwataka kukabidhi mihuri kwa watendaji wa mitaa na kumtaka waziri mwenye dhamana kutoa kauli ndani ya siku saba kuhusu mgogoro huo kabla awajafanya maamuzi ya kujihudhuru nchini nzima.

Wakizungumza katika mkutano na baadhi ya wawakilishi, wenyeviti hao wamewataka wakurugenzi wa halmashauri pia kuwaomba radhi wenyeviti wa mitaa kwa kuwa dharirisha ndani ya siku saba kwa maagizo waliyoyatoa kwa watendaji wa kata,na jeshi polisi na kusisitiza kama hawatekeleza maagizo hayo ndani ya muda husika watalazimika kujihudhuri ili kutoa fursa kwa serikali kuitisha uchaguzi mwingine nchini nzima.
 
Awali baadhi ya wenyeviti wa serikali za mitaa wamegoma kutekeleza agizo la kurejesha mihuri kwa watendaji wa mitaa kwa madai hawana uwezo wa kutoa huduma kwa wananchi kwa kuwa hawaishi katika maeneo hayo,na kususitiza lengo la serikali ya awamu ya tano ni kuondoa kero kwa wananchi kwa kutoa huduma bora na ndio maana wenyeviti hao wameendelea kutoa huduma kwa wananchi usiku na mchana. 
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Wakulima kulazimishwa kuuza korosho kinyume na bei elekezi. Je ni utawala bora?
Ndio
Hapana
Vote Now
Results
Weather