Independent Television Ltd
NHIF kufuta vibali kwa vituo vya afya ambavyo watumishi wake watatumia lugha chafu.

Uongozi wa mfuko wa taifa wa bima ya afya NHIF umetangaza kuchukua hatua kali ikiwa ni pamoja na kufuta vibali kwa vituo vya kutolea huduma za afya ambavyo  vitabainika watumishi wake kutumia lugha chafu,kashfa na kuwatenga wagonjwa wanaotibiwa kupitia utaratibu wa bima ya afya.

Kauli hiyo imetangazwa mjini Musoma mkoani mara na Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa mfuko wa taifa wa bima ya afya NHIF Bi Anne Makinda,wakati akizungumza na wadau mbalimbali wa mfuko huo wakiwemo viongozi na watendaji wa serikali mkoani Mara.
 
Naye Mkuu wa mkoa wa Mara Dk Charles Mlingwa,akizungumza wakati akifungua mkutano huo mkubwa,amekiri kuwa kuna baadhi ya wadau ambao wameshindwa kuwa wahaminifu na kufanya vitendo vya kuhujumu dhidi mfuko huo.
 
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi mkuu wa NHIF Bw Bernard Konga,amesema hivi sasa mfuko huo unapitia katika maboresho makubwa ambayo yatawezesha kuondoa vikwazo kwa wanachama wanaopata huduma kupitia mfuko huo.
 
 
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Kuelekea uchumi wa viwanda. Je mfumo wa elimu umebadilika kujibu mahitaji ya nchi
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather