Independent Television Ltd
Raia nane wa China washikiliwa na wizara ya kazi na ajira kwa kufanya kazi nchini bila vibali.

Raia nane wa kichina wameshikiliwa na wizara ya kazi,ajira,vijana na watu wenye ulemavu katika ziara ya kushtukiza iliyofanywa na naibu waziri wa wizara hiyo Mh. Anthony Mavunde katika viwanda viwili hapa jijini Dar es Salaam na kubaini hawana vibali halali vya kufanya kazi hapa nchini.

Zoezi hilo la kushtukiza limefanywa na naibu waziri wa kazi,ajira,vijana na watu wenye ulemavu Mh Athony Mavunde akiongozana na maafisa kutoka wizarani pamoja maafisa kutoka ofisi za wakala wa afya na usalama mahala pa kazi-osha katika viwanda viwili mali ya raia wa China,ambapo katika kiwanda cha Wen xing kilichopo Tegeta jijini Dar es Salaam,kabla ya Mh naibu waziri kutoa maagizo na kuwashikiliwa wachina wanne upande wa kiwanda hicho haya yakaibuka.
 
Katika kiwanda cha Shuntao kilichopo Mikocheni raia wanne walishiliwa kwa kuwa na vibali visivyo halali.
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Maandalizi ya timu za taifa katika mashindnao ya kimataifa. Je yamewekewa utaratibu kupata timu bora?
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather