Independent Television Ltd
Waziri mkuu amewataka viongozi kutowatangaza watuhumiwa wa dawa za kulevya bila ya kufanya uchunguzi.

Akizundua baraza la taifa la kudhibiti dawa za kulevya, Mheshimiwa Majaliwa licha ya kupongeza jitihada zinazofanywa na wakuu wa mikoa na wilaya katika kampeni ya kupambana na dawa za kulevya ametaka watuhumiwa wa dawa za kulevya watangazwe hadharani baada ya kujiridhisha ushiriki wao.

Mhe Majaliwa amesema baraza hilo halihitaji mtu yeyote mwenye mamlaka ya kufanya kazi ya kupambana na dawa za kulevya kupokea rushwa dhidi ya wafanyabiashara au watumiaji wa madawa ya kulevya.
 
Kuhusu ushiriki wa wananchi katika kampeni hiyo Mhe Majaliwa amewataka kutoa ushirikiano  kwa serikali katika mapambano dhidi yao ikiwa ni pamoja na kuacha kushiriki katika kutumia,au kuuza madawa ya kulevya ili kukwepa mkono wa sheria.
 
Aidha amesema tatizo la dawa za kulevya nchi ni kubwa kutokana na takwimu kuonyesha katika kipindi cha mwezi januari 2015 hadi desemba 2016 vyombo vya dola vimekamata kiasi cha kilo 77 za heroin,zilizohusisha kesi mia 703 na kilo 32.2 za cocaine zilizohusisha kesi 259, pamoja na kilo milioni 78 laki 6 na 56 za bangi zikihusisha kesi elfu 14 na mia tatu.
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Kuelekea uchumi wa viwanda. Je mfumo wa elimu umebadilika kujibu mahitaji ya nchi
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather