Independent Television Ltd
Polisi linawashikilia abiria pamoja na waendesha pikipiki zaidi ya 6 kwa kupanda pikipiki bila ya kuwa na kofia ngumu.

Jeshi la polisi limewakata abiria pamoja na waendesha pikipiki zaidi  ya 65 na kuwafikisha mahakamani kwa kufanya makosa mbalimbali ya barabarani  ikiwemo kupanda pikipiki bila ya kuwa na kofia ngumu ambapo jeshi hilo limesema kwa sasa halitatoza tena faini na  badala yake watuhumiwa watafikishwa mahakamani ili watu wabadilike.

Akizungumza na kituo kikuu cah polisi mkoa wa Temeke mkuu wa kikosi cha usalama barabrani kanda maalum ya Dar es Salaam  kamanda Haji  Awadhi  amesema waendesha boda boda wamekuwa wagumu kuelewa na hivyo ni muda mwafaka kuwabana.
 
Naye kamanda wa polisi  mkoa wa Temeke Giles Muruto amesema  watafanya oparesheni katika maeneo mbalimbali ya Temeke na watakaobainika watachukulia hatua  kali.
Baadhi ya watu waliokamatwa wamekuwa na maoni tofauti wengine wakikiri kutenda makosa na wengine wakisema wameonewa.
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Maandalizi ya timu za taifa katika mashindnao ya kimataifa. Je yamewekewa utaratibu kupata timu bora?
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather