Independent Television Ltd
Watu sita wanashikiliwa na Polisi wakituhumiwa kuuza na kusambaza dawa za kulevya aina ya Cocaine jijini Mbeya.

Watu sita akiwemo mfanyabiashara maarufu wa dawa za binadamu jijini Mbeya Steven Samwel Alliance maarufu kwa jina la Maranatha, wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa madai kuwa ni wauzaji na wasambazaji wakubwa wa dawa za kulevya aina ya Cocaine huku watu wengine 33 nao wakishikiliwa na jeshi hilo kwa tuhuma za kujihusisha na utumiaji wa dawa za kulevya.

Vita dhidi ya dawa za kulevya ambayo imeshika kasi nchini sasa imetua jijini Mbeya, ambapo kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, naibu kamishna wa jeshi la polisi, Dhahir Athuman Kidavashari amesema jeshi hilo linawashikilia watu sita ambao wanadaiwa kuwa ni wauzaji na wasambaji wakubwa wa dawa za kulevya jijini Mbeya.
 
Katika hatua nyingine kamanda Dhahir Athuman Kidavashari amesema katika mwendelezo wa jeshi la polisi kupambana na uhalifu, askari wake wamefanya msako katika maeneo mbalimbali jijini Mbeya na kufanikiwa kukamata wauzaji wa gongongo pamoja mali za wizi zikiwemo computer 11 ambazo zinadaiwa kuibwa katika chuo cha utumishi wa umma jijini Mbeya.
 
Kamanda Kidavashari amesema kukamatwa kwa watuhumiwa hao kunatokana na ushirikiano mzuri ambao jeshi hilo limeupata kutoka kwa wasamalia wema, hivyo ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalivu ili hatua ziweze kuchukuliwa.
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Kuelekea uchumi wa viwanda. Je mfumo wa elimu umebadilika kujibu mahitaji ya nchi
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather