Independent Television Ltd
Wachimbaji wadogo wa dhahabu waandamana kupinga agizo la kuwataka wawe na vyoo wilayani Mpanda.

Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu waliokuwa wakifanya shughuli za uchimbaji katika msitu wa Msaginya uliopo katika halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi wamefanya maandamano kwenda kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya ya Mpanda kupinga agizo la mkuu huyo kuwanyima kuendelea kuchimba katika eneo hilo kwa sababu za kutokuwa na vyoo na kuhatarisha afya zao huku kukiwa na watu wengine wakiendelea kuchimba kwa madai ya kuwa na vibali vya uchimbaji.

Wakizungumza ITV  wachimbaji hao ambao walizuiwa kuendelea kuchimba madini wiki moja iliyopita mpaka mazingira yatakapoboreshwa katika eneo hilo wamedai kuwa serikali haitendi haki kwa kuwaondoa na kuwapa vibali vya uchimbaji watu wengine kwa kuwa wao ndio waliogundua uwepo wa madini ya dhahabu katika eneo hilo.
 
Mkuu wa wilaya ya Mpanda Bi. Liliani Matinga amesema wamelazimika kuwazuia wachimbaji wadogo zaidi ya mia nne waliokuwa wamevamia na kuchimba katika kuvamia eneo la msitu wa Msaginya kinyume na madai ya wachimbaji hao.
 
Kwa upande wake anayedaiwa kuwa mmoja wa wamiliki wenye kibali cha kuchimba katika eneo hilo amesema bado hawajaanza shughuli za uchimbaji kwani wapo katika hatua za maandalizi ya  mgodi.
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Kuelekea uchumi wa viwanda. Je mfumo wa elimu umebadilika kujibu mahitaji ya nchi
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather