Independent Television Ltd
Shughuli za kibinadamu zatishia kukauka kwa vyanzo vya maji wilayani Mvomero.

Shughuli za kibinadamu zinazofanywa kandokando ya vyanzo vya maji zinatishia kukauka kabisa kwa mito miwili ya  Mlali na Mgera iliyopo wilayani Mvomero ambayo imekuwa ikitiririsha maji yake kwenda katika bwawa la Mindu  linalotegemewa kama chanzo kikuu cha maji kwa wakazi wa Morogoro.

ITV imetembelea maeneo hayo na kushuhudia kilimo pembezoni kabisa mwa mito hiyo, huku uchepushaji wa maji kwa kutumia mifereji midogo kando mito ukiwa umefanywa na wakulima ambapo  imewalazimu ofisi ya mkuu wa wilaya ya Mvomero kwa kushirikiana na mamlaka ya maji ya bonde la Wami Ruvu kushirikiana kurudisha maji yaliyochepushwa  katika mkondo huku afisa wa maji wa bonde la hilo Grace Chitanda akikiri shughuli hizo zimekuwa chanzo kikubwa cha uharibifu mkubwa na kwamba awali walishapanda mikonge kandokando ya mito hiyo lakini imekuwa ikivunjwa kwa makusudi na wananchi.
 
Kufuatia uharibifu huo,mkuu wa wilaya ya Mvomero Mohamed Utaly amepiga marufuku shughuli za kilimo kando kando ya mito hiyo na vyanzo vingine vya maji kuanzia septemba mwaka huu baada ya kuvunwa kwa mazao yaliyopandwa na watakaokiuka na kuendelea,hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
 
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Utaratibu wa viongozi kukutana na wananchi kusikiliza kero zao. Je, utasaidia kuongeza uwajibikaji kwa watendaji serikalini?
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather