Independent Television Ltd
Wasomi waombwa kuendeleza na kukuza lugha ya kiswahili barani Afrika.

Mjadala mkali umeibuka kuhusu matumizi ya lugha ya kiswahili ambapo wasomi wamekuwa na mitazamo tofauti huku wengine wakiunga mkono lugha ya Kiswahili kutumika kufundishia ngazi mbalimbali za elimu hapa nchini.

Miongoni mwa wasomi waliotoa mitizamo yao kuhusu lugha ya Kiswahili kutumika kufundishia ni Prof Kitila Mkumbo ambapo amesema tafiti zinaonyesha tatizo la elimu nchini halitokani na lugha ya kufundishia huku Dkt. Bashir Ally akisema lugha ya kiswahili inafaa kutumikan katika harakati za ukombozi wa Afrika.
 
Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo la matumizi ya kiswahili wameonyesha nia yao ya kutaka lugha ya kiswahili kutumika kufundishia katika nyanja mbalimbali,huku Prof. Abdallah Safari akisema licha ya tafiti nyingi kufanywa watafiti wamekuwa wakipuuzwa.
 
Balozi wa kiswahili Afrika mke wa rais wa awamu ya nne mama Salma Kikwete amebainisha hatua kubwa zilizofanywa na viongozi wa kiserikali katika kukikuza kiswahili, na kusema ni muda muafaka sasa kwa lugha ya kiswahili kupewa muda zaidi ili kiweze kukua zaidi.
 
Kongamano hilo la matumizi ya lugha ya kiswahili lililoandaliwa na chuo kikuu cha Dar es Salaam kupitia taasisi ya taaluma za kiswahili kwa kushirikiana na chama cha waandishi wa habari za Kiswahili Afrika ya mashariki kanda ya Tanzania lilijikita kujadili  uamuzi wa kutumia lugha ya Kiswahili katika nyanja mbalimbali nchini Tanzania je ni wakati muafaka.
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Utaratibu wa viongozi kukutana na wananchi kusikiliza kero zao. Je, utasaidia kuongeza uwajibikaji kwa watendaji serikalini?
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather