Independent Television Ltd
Chama cha madaktari wa afya ya kinywa na meno wafanya matembezi kuhamasisha umuhimu wa afya ya kinywa Dodoma.

Chama cha madaktari wa afya ya kinywa na meno nchini (TDA) kimefanya matembezi ya kuhamasisha wakazi wa Dodoma na taifa kwa ujumla kutambua umuhimu wa afya ya kinywa na meno kutokana na maradhi hayo kutopewa kipaumbele huku yakizidi kuongezeka kwa sababu mbalimbali ikiwemo uvutaji wa tumbaku ulaji wa vyakula vyenye sukari nyingi pamoja na jamii kutofahamu njia sahihi za kufanya usafi wa kinywa.

Matembezi hayo yaliyoanzia kwenye viwanja vya Nyerere na kuzunguka katika mitaa mbalimbali ya mji wa Dodoma na kisha kumalizikia kwenye viwanja hiyo yamehusisha watu wa kada mbalimbali ikiwemo viongozi wa serikali wanasiasa wananchi na wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ambapo rais wa TDA Dkt. Lorna Carneiro amesema ipo haja ya kuhimiza jamii kuhusu afya bora ili kupunguza magonjwa ya kinywa na meno.
 
Kwa upande wake daktari wa kinywa na meno wa mkoa wa Dodoma Dkt. Samwel Seseja amesema bado kuna changamoto kubwa kwa matibabu ya kinywa na meno hasa maeneo ya vijijini kutokana na uhaba wa wataalamu wa matibabu hayo, ukosefu wa uwiano wa vifaa tiba na vitendea kazi kwa wagonjwa huku vifaa vilivyopo vikiwa duni ambavyo havikidhi kutoa huduma .
 
Naye naibu waziri ofisi ya waziri mkuu sera bunge ajira vijana na watu wenye ulemavu Mhe Anthony Mavunde amewataka wananchi kuepuka tabia hatarishi kwa afya ya kinywa na meno ikiwemo uvutaji tumbaku, unywaji pombe kupitiliza pamoja na kufanya uchunguzi wa mara kwa mara kuhusu afya ya kinywa na meno .
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Kuelekea uchumi wa viwanda. Je mfumo wa elimu umebadilika kujibu mahitaji ya nchi
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather