Independent Television Ltd
Rais Dkt. Magufuli aweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara za mapishano ya juu eneo la Ubungo DSM.

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Daktari John Pombe Magufuli ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara za mapishano ya juu katika makutano ya barabara,Morogoro,Mandela na Sam Nujoma yaliyopo eneo la Ubungo na kuzitaka mamlaka husika kukamilika kwa wakati mradi huo ili kuwaondolea hadha ya foleni kwa watumiaji wa barabara hizo.

Akizungumza katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi barabara hizo, rais Magufuli ameitaka wizara ya ujenzi,uchukuzi na mawasiliano kwa kushirikiana na mkandarasi wa mradi huo kuhakikisha wanamaliza mradi huo katika kipindi cha miezi 20 badala ya miezi 30 iliyotajwa na wakala wa barabara nchini-TANROAD.
 
Aidha Dkt Magufuli amenwakikishia rais wa benki ya dunia kuwa serikali ya Tanzania ilipa mikopo kwa majIbu wa makubaliano ili kujenga uaminifu na kuifanya Tanzania kuweza kukopesheka zaidi ambapo amesema benki ya dunia imeikopesha Tanzania zaidi ya shilingi trilioni 1.74 mikopo ambayo riba yake ni nafuu na inalipika.
 
Awali akimkaribisha rais, waziri wa ujenzi,uchukuzi na mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema mradi huo unajengwa kwa gharama ya shilingi bilionbi 188.71 ambapo kati ya fedha hizo shilingi bilioni 177.4 zinatumika katika ujenzi, huku shilingi bilioni 9 zinatumika katika usanifu ambapo kwa ajili ya fidia serikali imelipa zaidi ya shilingi bilioni 1.9.
 
Kwa upande wake rais wa benki ya dunia Daktari Jim Yong Kim amesema amepongeza serikali ya Tanzania kwa kudhibti rushwa ambapo amesisitiza uongozi imara na thabiti ni muhimu kwa maendeleo kwa sababu hata fedha za misaada toka nje lazima isimamiwe na uongozi ambao ni imara na unalenga kuleta mageuzi ya kweli ikiwemo kufikia nchi ya uchumi wa kati ifikapo 2015.
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Kuelekea uchumi wa viwanda. Je mfumo wa elimu umebadilika kujibu mahitaji ya nchi
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather