Independent Television Ltd
Waziri Mh.Nape Nnauye amelaani kitendo cha Mkuu wa mkoa wa DSM kuvamia ofisi za Clouds Media.

Waziri wa habari,utamaduni,sanaa na michezo  Mh Nape Nnauye amelani tukio la mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda la kuvamia ofisi za Clouds Media jijini Dar es Salaam siku ya ijumaa usiku na kwamba tukio hilo limeweka doa uhuru wa vyombo vya habari hapa nchini katika kutekeleza wajibu wao.

Akizungumza na vyombo vya habari katika ofisi za Clouds Media Mikocheni jijini Dar es Salaam,waziri wa habari,utamaduni,sanaa na michezo Nape Moses Nnauye akiongozana na baadhi ya viongozi kutoka TCRA,mkurugenzi wa habari maelezo na mwenyekiti wa chama cha wamiliki wa vyombo vya habari Tanzania Dr. Reginard Mengi ambapo mbali na kuwapa pole uongozi na wafanyakazi wa Clouds Media kwa kile kilichotokea,Nape amesema kama serikali wanakilani tukio hilo kwa nguvu zote.
 
Kutokana na tukio hilo,waziri Nape Nnauye akalazimika kuunda kamati ya watu watano watakaofanya kazi hiyo kwa saa 24 ili kutoa nafasi ya kamati hiyo kupata maelezo ya upande wa pili ili wa mkuu wa mkoa wa DSM naye apewe nafasi ya kujieleza.
 
Aidha mwenyekiti wa MOAT ameomba hatua zichukuliwe baada ya kamati hiyo kumaliza kusikiliza upande wa pili.
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Kuelekea uchumi wa viwanda. Je mfumo wa elimu umebadilika kujibu mahitaji ya nchi
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather