Independent Television Ltd
Waziri mkuu wa zamani wa Israel afurahishwa namna Tanzania inavyotekeleza sera ya uhifadhi wa maliasili na mambo ya kale.

Waziri Mkuu wa zamani wa Israel Ehud Barack ametembelea Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na kulitaja Bonde la Olduvai Gorge kulipogundulika fuvu la binadamu wa kwanza kuwa ni eneo muhimu la kumbukumbu ya uso wa dunia na kwamba amefurahishwa na namna Tanzania inavyotekeleza sera ya uhifadhi wa maliasili pamoja na mambo ya kale.

Akizungumza ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro akiwa katika ziara binafsi huku akiambatana na ujumbe mzito wa watalii kutoka nchini Israel Ehud Barack ambaye anatembelea Ngorongoro na Hifadhi ya Serengeti amesema amefurahishwa na namna Tanzania inavyotoa kipaumbele kwenye masuala ya uhifadhi ukilinganisha na nchi zingine barani Afrika.
 
Naibu Waziri wa mali asili na utalii Mhandisi Ramo Makane ambaye alipata fursa ya kukutana na Ehud Barack amesema Tanzania inamatumaini ya kupata watalii wengi zaidi kutoka Israel hali inayotokana ujio watu maarufu kama Ehud Barack. 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Utaratibu wa viongozi kukutana na wananchi kusikiliza kero zao. Je, utasaidia kuongeza uwajibikaji kwa watendaji serikalini?
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather