Independent Television Ltd
Waziri Mhe. Mwigulu Nchemba aongoza maafisa wa polisi na mamia ya wananchi kuaga miili ya askari waliouawa mkoani Pwani.

Waziri wa mambo ya ndani Mhe. Mwigulu Nchemba ameongeza maafisa wa polisi na mamia ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam kuaga miili ya askari waliouwawa katika shambulio na watu wasiojulikana Kibiti mkoani Pwani.

Mhe. Mwigulu Nchemba licha ya kutoa pole kwa familia za marehemu amesema serikali haitafumbia macho matukio hayo ambayo yameendelea kugharimu maisha ya maofisa wa usalama wa raia na kuwataka wananchi wa maeneo hayo kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kufanikisha azma yake ya kuwakamata waliotekeleza tukio hilo la kinyama.
 
Baadhi ya wananchi walioshiriki katika tukio la kuaga miili hiyo licha ya kulaani kitendo hicho wamelitaka jeshi la polisi kuwa karibu na wananchi ili kuweza kubaini kama kuna tatizo katika jamii hiyo na kuweza kuzuia matukio kama hayo kabla ya kutokea.
 
Tukio hilo lilitokea juzi tarehe 13 april mwaka huu katika eneo la Kibiti mkoa Pwani ambapo askari hao walivamiwa na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi na kusababisha mauaji hayo.
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Utaratibu wa viongozi kukutana na wananchi kusikiliza kero zao. Je, utasaidia kuongeza uwajibikaji kwa watendaji serikalini?
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather