Independent Television Ltd
Wachimbaji wadogo zaidi ya 300 waandamana wakiilalamikia serikali kuwaondoa kumpisha mwekezaji mkoani Shinyanga

Wachimbaji wadogo zaidi ya 300 wa kitongoji cha Mahiga kata ya Mwakitolyo wilayani Shinyanga wameandamana na kukusanyika wakiwa wamebeba mabango yanayoitaka serikali itoe tamko la wazi juu ya uwepo wa mwekezaji wa kichina anayedaiwa kuwepo katika eneo lao la machimbo ya madini ya dhahabu.

ITV imefika katika eneo hilo la Mahiga na kushuhudia wachimbaji hao wakiwa wamekusanyika huku wakilalamikia serikali ya mkoa wa Shinyanga kutoa siku saba kuondoka na kupisha shughuli za mwekezaji aliye na leseni ya uchimbaji wa madini jambo ambalo wamelipinga na kuitaka serikali itoe tamko la wazi.
 
Diwani wa kata ya Mwakitolyo Mhe.Limba Agastin amedai kuwa matamko tofauti tofauti yanayotolewa na viongozi wa serikali yamesababisha watendaji kufanya kazi katika mazingira magumu huku wananchi wakiwatuhumu kuhusika na rushwa kutoka kwa wawekezaji wanaotajwa kuwa na leseni ya uchimbaji.
 
Hata hivyo ITV imemtafuta mkuu wa mkoa wa Shinyanga kutaka kujua juu ya malalamiko ya wachimbaji hao na kudai kuwa eneo lililoachiwa litumiwe na wachimbaji wadogo ni eneo la Nyaligongo kuanzia namba 2 hadi namba tano lenye zaidi ya kilomita 15.5 lakini eneo la Mahiga lina leseni ya mwekezaji huku kamishna msaidizi wa madini kanda ya magharibi mhandisi Hamisi Kamando akitoa ufafanuzi juu ya leseni hiyo.
 
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Utaratibu wa viongozi kukutana na wananchi kusikiliza kero zao. Je, utasaidia kuongeza uwajibikaji kwa watendaji serikalini?
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather