Independent Television Ltd
Wizara ya afya kupanua wigo wa kusambaza dawa za kuwasaidia walioathirika na dawa za kulevya.

Wizara ya Afya,Maendeleo ya jamii,jinsia wazee na watoto,imeanza mchakato wa kupanua wigo wa kusambaza dawa za kuwasaidia waathirika wa dawa za kulevya nchini katika mikoa mitano Tanzania bara kufuatia nguvu kazi katika maeneo hayo kuathirika kwa sababu ya matumizi hayo.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto katika uzinduzi wa jengo la kuhudumia afya ya akili lililojengwa kwa hisani ya serikali ya Norway kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 500 ili kupunguza athari kwa waathirika wa tatizo hilo,Daktari mkuu wa serikali Profesa Muhamad Kambi ameitaja mikoa itakayohusika na zoezi hilo kuwa ni Tanga, Mbeya, Dodoma, Kilimanjaro na Arusha.
 
Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na Balozi wa Norway nchini,viongozi wa dini pamoja na wataalam wa afya aya akili kutoka Norway,Mganga mkuu wa mkoa wa Tanga Dr,Aisha Mahita amesema takwimu zilizokusanywa katika mkoa wake,zinaonesha kuwa wagonjwa walioathirika na afya ya akili ni zaidi ya 8,000 ambapo kati hao walioathirika na dawa za kulevya ni zaidi ya 930 huku wanaume wakiwa 864 na wanawake .
 
Kufuatia hatua hiyo Mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shigella ameziagiza mamlaka husika kuhakikisha kuwa wanaimarisha ulinzi na doria katika mipaka inayounganisha nchi jirani ya kenya pamoja na maeneo ya bahari ya Hindi inayotumika kupitisha dawa hizo na kuathiri nguvu kazi ya taifa .
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Utaratibu wa viongozi kukutana na wananchi kusikiliza kero zao. Je, utasaidia kuongeza uwajibikaji kwa watendaji serikalini?
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather