Independent Television Ltd
Ndugai awaongoza wabunge kuaga mwili wa marehemu Elly Macha Dodoma.

Spika wa Bunge Mhe.Job Ndugai amewaongoza wabunge,wafanyakazi wa bunge na mamia ya wakazi wa mkoa wa Dodoma katika kuuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia cha ma cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA Dr.Elly Macha aliyefariki nchini Uingereza March 31 akiwa katika  matibabu.

Akizungumza katika ibada kabla ya  kuanza  kuagwa kwa  mwili wa marehemu Dr.Macha,Mchungaji wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania aliyeongoza ibada hiyo Samwel Mshana amesema wao viongozi wa dini wamekuwa wakiwaombea viongozi wa ngazi mbalimbali ili kuwafanya wawe na hekima katika maamuzi yao kwa manufaa ya taifa.
 
Naye Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai amesema  Dr.Macha ameacha pengo bungeni kwani alikuwa mstari wa mbele katika kudai  maslahi ya jamii nzima hasa ya walemavu huku Waziri Mkuu Mhe.khasim Majaliwa akisema serikali itayaendeleza yale yote ambayo Marehemu Dr.Elly Macha alikuwa akiyapigania enzi za uhai wake.
 
Naye kiongozi wa Kambi ya upinzani bungeni Mhe.Freeman Aikaeli Mbowe  amewataka wabunge kubadilika na kuwa na upendo baina yao nyakati zote bila kujali vyama vyao  kama ambavyo walivyofanya katika msiba huo wa marehemu Dr.Elly Macha na kuacha kuwa na chuki ambazo zimekuwa hazina tija.
 
Dr.Elly Marko Macha alifariki akiwa katika matibabu kwenye hospitali ya  New Cross wolverhampton iliyopo nchini Uingereza akikabiliwa na maradhi ya upungufu  wa damu na ameacha mtoto mmoja
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Utaratibu wa viongozi kukutana na wananchi kusikiliza kero zao. Je, utasaidia kuongeza uwajibikaji kwa watendaji serikalini?
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather