Independent Television Ltd
Wananchi mkoani Rukwa watakiwa kuchukua tahadhari zaidi juu ya ugonjwa hatari wa Ebola.

Jamii mkoani Rukwa inapaswa kutahadharishwa juu ya ugonjwa hatari wa Ebola, licha ya ugonjwa huo unaoenea kwa kasi kutokuwa na madhara kwa sasa,lakini kuthibitishwa kwake na Shirika la Afya duniani kuwa ugonjwa huo upo katika nchi ya jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na kuwepo na mwingiliano mkubwa wa watu kwenye vijiji zaidi ya 45 vilivyoko katika mwambao wa Ziwa Tanganyika, kunaiweka Rukwa katika hatari kubwa zaidi.

 Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa wa Rukwa Dakta Emmanuel Mtika, akiongea mjini Sumbawanga na madiwani wa kata zote 97 za halmashauri zote nne za mkoa huo, amesema kuna umuhimu mkubwa kwa wananchi kujua juu ya kuwepo kwa ugonjwa huo katika nchi ya jirani DRC Congo, na kuwapatia elimu juu ya ugonjwa huo wa Ebola unaoenea kwa kasi na usiokuwa na tiba, ili kila waonapo dalili zozote hasa kwa watu wanaoingia nchini kwa njia ya majini, kutoa taarifa mapema ili hatua zichukuliwe haraka.
 
Naye mkuu wa mkoa wa Rukwa Bw Zelote Steven,akiongea na madiwani hao amesema Wizara ya afya, maendeleo ya jamii,jinsia wazee na watoto,imekuwa ikichukua hatua mbalimbali za kuboresha mikakati ya kudhibiti ugonjwa huo usiingie nchini,na kwamba wawakilishi hao wa watu  wasiende kuwatia hofu wananchi bali kuwapa tahadhari tu.
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Wakulima kulazimishwa kuuza korosho kinyume na bei elekezi. Je ni utawala bora?
Ndio
Hapana
Vote Now
Results
Weather