Independent Television Ltd
Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mwanza Sekou Toure haina mashine za CT SCAN na MRI.

Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mwanza Sekou Toure, inayotegemewa na wagonjwa wa mikoa jirani ya Kanda ya Ziwa, inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa mashine za CT SCAN na MRI, zinazotumika kwa ajili ya uchunguzi wa magonjwa ya mfumo wa fahamu na mifupa, uchakavu wa miundombinu pamoja na uhaba wa madaktari bingwa.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dk. Onesmo Rwakyendela, akizungumza kwenye uzinduzi wa bodi ya ushauri ya hospitali hiyo ameiomba Ofisi ya Rais TAMISEMI na wizara ya Afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto kuruhusu hospitali za mikoa kuingia ubia na taasisi binafsi ili ziweze kutoa huduma za vipimo vya CT SCAN na MRI.
 
Mganga Mkuu wa mkoa wa Mwanza Dk. Leonard Subi, mbali na kugusia Sakata la vyeti feki lililowakumba watumishi 12 kati ya 389 wa Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza Sekou Toure;waliopo kwenye kada mbalimbali, pia ametoa tahadhari kwa wananchi kuhusu ugonjwa wa Ebola ambao umeripotiwa kutokea katika nchi jirani ya DRC Congo.
 
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella,akizindua Bodi ya ushauri ya hospitali ya Rufaa ya mkoa huo,amekemea vitendo vya wizi wa dawa na vifaa tiba kwenye vituo vya kutolea huduma za afya vinavyodaiwa kufanywa na baadhi ya watumishi wasio waaminifu.
 
Hospitali hiyo inayohudumia zaidi ya wakazi milioni 3,ina vitanda 303 na wodi 9, pia ina madaktari bingwa wanne,madaktari wa kawaida 22,wauguzi wasajiliwa 190 na wataalamu wa maabara 16.
 
Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita,hospitali hiyo imeweza kuwahudumia wagonjwa wa nje zaidi ya laki tano katika huduma zilizohusisha vipimo vya mionzi,maabara na upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi pamoja na huduma za afya ya uzazi na watoto.
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Kuelekea uchumi wa viwanda. Je mfumo wa elimu umebadilika kujibu mahitaji ya nchi
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather