Independent Television Ltd
Mvutano waibuka ndani ya Baraza la wawakilishi Zanzibar

Naibu Spika wa Baraza la wawakilishi amejikuta katika wakati mgumu baada ya  mmoja ya mwakilishi kumtupia lawama kuwa anayumba  na kiti cha Spika kutokana na kutosikiliza kilio cha wananchi waliovunjiwa nyumba zao kwa amri ya Wizara ya Tawala za mikoa na vikosi vya SMZ.

Hali hiyo iliibuka wakati wa kupitisha Bajeti ya wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa,serikali za mitaa na idara maalum za SMZ ambapo wakati Naibu Spika  Mhe Mgeni Hassan Juma  alipokuwa akitaja vifungu vya wizara hiyo ndipo mwakilishi wa wananchi wa  Jimbo  la Paje  Mhe Jaku Ayoub aliposimama na kutaka hoja yake ya kuvunjiwa nyumba wananchi wa Kyanga  kutaka ijibiwe.
 
 
Hata hivyo waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa,serikali za mitaa na idara maalum za SMZ Mhe Haji Omar Kheri ambaye tokea juzi amekuwa akipambana na hoja za wawakilishi amesema serikali inawajali wananchi wake na nyumba hizo zimevunjwa kwa vile ziko ndani ya vyanzo vya maji na zimejengwa kinyume na utaratibu wa mipango miji ya serikali.
 
 
 Hatiamye wajumbe walipitisha  bajeti ya wizara hiyo  ambayo ni moja ya wizara inayugusa jamii moja kwa moja ilianza kujadiliwa tokea wiki iliyopita na kumalizika siku ya Alhamsi ambapo Waziri aliweza kukumbana na maswali ya barabara,mitaro na masuala ya vikosi vya SMZ.
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Kuelekea uchumi wa viwanda. Je mfumo wa elimu umebadilika kujibu mahitaji ya nchi
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather