Independent Television Ltd
Wanaotoa rambirambi kwa maadhura wa ajali ya basi la wanafunzi wafuate sheria na taratibu.

Wakati Meya wa  jiji la Arusha Bw Kalst Lazaro na watu wengine wanne wakiwa bado anahojiwa na polisi kuhusiana na tuhuma  za kutengeneza mkusanyiko usio na kibali serikali mkoani Arusha imewataka wananchi na taasisi zinazoendelea kutoa rambirambi kwa familia za wanafunzi waliofariki katika ajali ya basi la wanafunzi kufuata taratibu zilizowekwa ili kuepusha migongano isiyo ya lazima .

Akizungumza wakati anapokea misaada inayoendelea kutolewa na wadau mbalimbali Mkuu wa mkoa wa Arusha Bw Mrisho Gambo amesema  masuala ya fedha yana changamoto na yasiposimamiwa vizuri lengo tarajiwa haliwezi kutimia.
Aidha amesema serikali itaendelea kuwadhibiti wote watakaotaka kuingiza siasa kwenye majanga likiwemo la vifo  vya wanafunzi na amesisitiza umuhimu wa kila mmoja kufuata sheria  taratibu na maelekezo yanayotolewa  na  serikali.
Wakizungumza baada ya kukabidhi rambirambi zao baadhi ya wadau hao wamesema lengo lao ni kuungana na wadau   wengine katika kuwasaidia maadhura  wa ajali ya basi la wananfunzi.
 
Meya huyo wa jiji la Arusha na watu wengine wakiwemo waandishi wa habari,viongoziwa dini nabaadhi ya wananchi walikamatwa katika mkusanyiko unaodaiwa kuwa ulikuwa na lengo la kutoa rambirambi bila kufuata taratibu na hadi muda huu watu wengine wote walishahojiwa na kuachiliwa huru wakiwemo viongozi wa dini . 
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Kuelekea uchumi wa viwanda. Je mfumo wa elimu umebadilika kujibu mahitaji ya nchi
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather