Independent Television Ltd
Watu watatu wanaosadikiwa kuwa majambazi wameuawa katika majibizano ya risasi na polisi.

Watu watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi,wameuawa katika majibizano ya risasi na Jeshi la polisi mkoani Mwanza usiku wa kuamkia leo katika eneo la Igoma jijini Mwanza,ambapo katika eneo la tukio hilo polisi wamefanikiwa kupata bastola moja ikiwa na risasi 15 na magazini mbili na bunduki aina ya short gun ikiwa na risasi mbili pamoja na maganda mawili ya risasi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Naibu Kamishina Ahmed Msangi,amewataja waliouawa kuwa ni Benedicto Thobias mkazi wa Nyamatara Buhongwa,Mabula Segeja na Charles Thomas Garula ambao wamejeruhiwa kwa risasi na baadaye kufariki dunia wakati wakipelekwa hospitalini baada ya kurushiana risasi na askari polisi.
 
Miili ya washukiwa hao wa tukio la ujambazi,imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Bugando kwa ajili ya uchunguzi na utambuzi,huku msako wa kuwasaka wenzao wawili ambao wametoroka na wengine waliokuwa wanashirikiana nao ukiendelea kufanyika.
 
ITV imefika eneo la tukio na kuzungumza na baadhi ya wakazi wa mtaa wa Ndofye pamoja na Mbugani walioshuhudia majibizano ya risasi,baada ya watuhumiwa hao kukaidi amri ya kujisalimisha kwa hiyari.
 
Watuhumiwa hao wa ujambazi kabla ya kufikwa na mauti,inasemekana walianzia kwenye kituo cha mafuta cha Lake Oil kilichopo jirani na makaburi ya kumbukumbu ya MV.Bukoba ambako waliwaamuru wahudumu wa kituo hicho kujaza mafuta kwenye gari lao.
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Utaratibu wa viongozi kukutana na wananchi kusikiliza kero zao. Je, utasaidia kuongeza uwajibikaji kwa watendaji serikalini?
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather