Independent Television Ltd
Watumishi 72 wilayani Misungwi wasimamishwa kazi wakiwemo 68 wenye vyeti feki.

Halmashauri ya wilaya ya Misungwi mkoa wa Mwanza imewasimamisha kazi watumishi zaidi ya sabini wakiwemo wenye vyeti feki 68,wabadhilifu wa mali za umma wawili na watovu wa nidhamu wawili huku idara ya elimu na afya zikiathirika kwa kiwango kikubwa.

Amebainisha hayo Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Misungwi Bw.Athon Masele wakati akizungumza na ITV juu ya maendeleo ya wilaya ya Misungwi 
 
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Misungwi Mh.Charles Kitwanga amesema kuwa mwaka jana walisimamishwa kazi watumishi wawili kwa tuhuma za ubadhilifu wa mali za umma ambapo katika kipindi cha mwezi mmoja mapato yameongezeka kwa kiwango kikubwa kutoka kiasi cha shilingi milioni 24 hadi shilingi milioni 120 kwa mwezi hali iliyosaidia kupata hati safi baada ya cag kulidhishwa na utendaji kazi wa halmashauri
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Kuelekea uchumi wa viwanda. Je mfumo wa elimu umebadilika kujibu mahitaji ya nchi
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather