Independent Television Ltd
PTF umetoa zaidi ya shilingi Milioni 10 kwa vijana wakike waliyoweka ahadi ya kuachana na dawa za kulevya.

Mfuko wa Rais wa kujitegemea PTF umetoa zaidi ya shilingi Milioni 10 kwa vijana wakike waliyoweka ahadi ya kuachana na madawa ya kulevya ili waweze kujiingiza katika biashara halali.

Wasichana hao wa jijini Dar es Salaam  eneo la Kigogo awali walipewa mafunzo ya ujasiriamali na namna madawa ya kulevya yanavyowadhohofisha afya zao huku baadhi ya wasichana hao wakikiri kujiingiza katika madawa hayo na biashara nyingine haramu na sasa wameahidi kuachana na madawa hayo na kujikita zaidi katika ujasiriamali.
 
Akiongea katika hafla hiyo yakuwakabidhi fedha na vyeti vya ushiriki wa mafunzo Mkurugenzi wa mfuko huo uliyoko chini ya Ofisi ya Rais Bi Agatha Kitale amesema wimbi la wasichana kujiingiza katika biashara haramu limekuwa kubwa na jitidaha za Rais zitasaidia kuwapunguza na baadaye kumaliza tatizo hilo.
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Kuelekea uchumi wa viwanda. Je mfumo wa elimu umebadilika kujibu mahitaji ya nchi
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather