Independent Television Ltd
Kamati ya Bunge ya Serikali za mitaa yabaini ufujaji mkubwa wa fedha za umma.

Kamati ya Bunge ya Hesabu za mashirika ya umma  imesema hali ni mbaya katika miradi mingi inayoisimamiwa na mashirika ya umma ambayo imeikagua  na kubaini  ufujaji mkubwa wa fedha za umma  na kutaka hatua za kisheria kuchukuliwa kwa wahusika.

Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe.Naghenjwa Kaboyoka amesema hayo katika mkutano wa wadau wa taasisi zisizo za kiserikali uliokuwa ukijadili  Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya mwaka.
 
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za mitaa Mhe.Vedasto Ngombale amesema kamati hizo za Bunge zimekuwa zikishindwa kukagua miradi mingi ya maendeleo hasa yenye utata kutokana na kukosekana kwa fedha za kuitembelea.
 
Waratibu wa mkutano huo wamesema ni wajibu wa taasisi ambazo siyo za kiserikali kupitia ripoti hiyo ya CAG kwa kina na kisha kwenda kuwaeleza wananchi yaliyopo ili nao wao watumie nafasi yao kutaka mapungufu yanayobainika yawe yanafanyiwa kazi.
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Kuelekea uchumi wa viwanda. Je mfumo wa elimu umebadilika kujibu mahitaji ya nchi
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather