Independent Television Ltd
Waziri wa Usalama nchini Kenya, Jenerali Mstaafu JOSEPH NKAISSERY amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 67.

Waziri wa Usalama nchini Kenya, Jenerali Mstaafu JOSEPH NKAISSERY amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 67.

Waziri huyo amefariki dunia saa chache baada yake kulazwa katika hospitali binafsi ya Karen kufanyiwa uchunguzi.
 
Taarifa za kifo chake zimetangazwa na mkuu wa utumishi wa umma Bwana  JOSEPH KINYUA alfajiri ya leo.
 
Bwana KINYUA amesema Taifa litaendelea kupewa taarifa zaidi juu ya msiba huo wa habari zaidi za waziri huyo wa zamani wa Usalama wa nchini Kenya.
 
Waziri huyo alizaliwa mwaka 1949 na alihudumu katika jeshi kwa miaka 29 kabla ya kuingia katika siasa wakati wa uchaguzi wa mwaka 2002 ambapo alimshinda David Sakori wa chama cha KANU wakati wa kustaafu kwa Rais Daniel arap Moi katika eneo bunge la Kajiado ya Kati.
 
Wakati huo huo,  Rais UHURU KENYATTA amemteua Waziri wa Elimu Dakta  FRED MATIANG'I kukaimu nafasi ya Waziri wa Usalama wa Ndani kufuatia kifo cha aliyekuwa waziri wa wizara hiyo, Jenerali Mstaafu JOSEPH NKAISSERY.
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Utaratibu wa viongozi kukutana na wananchi kusikiliza kero zao. Je, utasaidia kuongeza uwajibikaji kwa watendaji serikalini?
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather