Independent Television Ltd
Serikali imeziagiza mamlaka za miji nchini kuwavunjia watakaojenga maeneo yasiyopimwa.

Serikali imeziagiza mamlaka za miji nchini kuwavunjia mara moja watu ambao wananzisha ujenzi katika maeneo ambayo hayajapimwa kwani kwa sasa Serikali imeweka mazingira rafiki ya watu kumiliki ardhi.

Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi Mhe.Willium Lukuvi ametoa agizo hilo mara baada ya kutembelea taasisi ambazo zipo chini ya wizara yake na zinashiriki maonesho ya biashara ya Dar es Salaam.
 
Nao baadhi ya wasimamizi wa Taasisi hizo ambazo ni Shirika la Nyumba la Taifa na kampuni ya Nyumba ya Watumishi wamesema wamekuwa wakifanya kazi zao kwa weledi ili kuwapatia Watanzania makazi bora.
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Kuelekea uchumi wa viwanda. Je mfumo wa elimu umebadilika kujibu mahitaji ya nchi
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather