Independent Television Ltd
Watu wenye uwezo nchini wametakiwa kuisaidia serikali kuboresha utoaji wa elimu nchini.

Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dr Reginald MENGI ametoa rai hiyo  Mkoani Kilimanjaro wakati wa hafla ya kuwazawadia wanafunzi 47 wa shule ya sekondari ya wasichana Ashira shilingi Bilioni moja kila mmoja,baada ya kufaulu kwa daraja la kwanza katika mtihani wa taifa wa kidato cha sita, Ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa wakati wa mahafali yao mwaka jana.

Dr Mengi,ambaye pia ametekeleza ahadi yake ya kuchangia shilingi milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa ukuta wa shule hiyo,amempongeza Rais John Pombe Magufuli kwa jitihada zake za  kutoa  elimu bure nchini.
 
Dr Mengi pia ameahidi kumzawadia shilingi milioni moja na laki moja kila mhitimu wa kidato cha sita wa shule hiyo mwaka huu atakayefaulu kwa daraja la kwanza katika mtihani wa taifa.
 
Mapema Mwenyekiti wa Bodi ya Shule Askofu Mstaafu Dr Martin Shao,MKUU wa Shule hiyo Mwalimu Elizabert Abdallah na Mwakilishi wa Wazazi Bw.Julius Sanga walimpongeza Dr MENGI kwa moyo wake wa kusaidia jamii.
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Ongezeko la makosa ya barabarani .je ni udhaifu katika usimamizi wa sheria .
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather