Independent Television Ltd
Ndege aina ya Kweleakwelea washambulia Mtama mikoa ya Lindi na Dodoma.

Wizara ya kilimo na umwagiliaji  imeombwa kuweka kipaumbele cha  kukabiliana na ndege waharibifu aina ya Kweleakwelea wanaoshambulia zao la Mtama aina ya Baraka na Masia mbegu ambayo imeonyesha  kufanya vizuri katika mikoa ya kusini na kanda ya kati ikiwemo mkoa wa Dodoma na hivyo kurudisha nyuma juhudi za wakulima katika kupanda mazao yanayostaimili ukame.

Akizungumza na ITV iliyotembelea mikoa ya Lindi na Dodoma  afisa kilimo wa halmashauri ya wilaya ya Bahi Jovin Barabata amesema ndege aina ya Kweleakwelea ni tatizo kubwa katika wilaya yake  licha ya wizara ya kilimo na umwagiliaji kukabiliana nao.
 
Kwa upande wao baadhi ya wakulima wanaolima zao hilo kutoka mikoa ya Lindi na Dodoma wanasema licha ya mbegu hizo kufanya vizuri mashambani  ndege waharibifu ni tatizo lakini pia masoko ni shida na hivyo baadhi yao kutumia kulisha mifugo.
Mbegu za mtama aina ya  Baraka na Masia  zimegunduliwa na taasisi ya utafiti wa kilimo Naliendele na zimeonyesha kufanya vizuri hasa katika maeneo yenye ukame.
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Utaratibu wa viongozi kukutana na wananchi kusikiliza kero zao. Je, utasaidia kuongeza uwajibikaji kwa watendaji serikalini?
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather