Independent Television Ltd
Wananchi wapinga ujenzi wa kiwanda karibu na Zahanati manispaa ya Sumbawanga.

Wakazi wa maeneo ya Mjimwema katika kata ya Malangali kwenye manispaa ya Sumbawanga, wamepinga vikali ujenzi unaoendelea wa kiwanda cha kusindika nafaka, jirani kabisa na Zahanati ya Malangali kinyume cha utaratibu, hali itakayoathiri utendaji wa zahanati hiyo na afya za wagonjwa.

Wananchi hao wa kata ya Malangali wakiongea mbele ya mbunge wa Sumbawanga mjini Mheshimiwa Aeshi Hilal, wamesema kiwanda hicho cha kusindika nafaka kikianza kufanya kazi, kitaathiri mno hali za wagonjwa wanaopata huduma kwenye zahanati hiyo, ikiwa ni pamoja na akina mama wajawazito wanaotegemea kujifungulia hapo, kwa hali hiyo ujenzi huo haupaswi kuendelea kabisa.
 
Akizungumza na wananchi hao mbunge wa Sumbawanga mjini Mheshimiwa Aeshi Hilal, amesema licha ya serikali ya awamu ya tano kuhimiza ujenzi wa viwanda nchini, lakini ujenzi huo ni lazima uzingatie sheria na taratibu zote za afya na mazingira kwa ujumla, na hasa ikizingatiwa kuwa manispaa hiyo imeshatenga tayari maeneo ya uendelezaji wa viwanda.
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Kuelekea uchumi wa viwanda. Je mfumo wa elimu umebadilika kujibu mahitaji ya nchi
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather