Independent Television Ltd
Shule ya msingi Kingili inakabiliwa na uhaba wa vyumba vya madarasa nakusababisha wanafunzi kusoma wakiwa wamesongamana.

Shule ya msingi Kingili iliyopo kata ya Ntaba, halmashauri ya Busokelo wilayani Rungwe, inakabiliwa na uhaba mkubwa wa vyumba vya madarasa ambapo kati ya vyumba 24 vinavyohitajika, kwa sasa ina vyumba vinne tu, hali ambayo inasababisha wanafunzi kusoma wakiwa wamesongamana madarasani. 

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya vyumba vitatu vya madarasa ambavyo vimejengwa shuleni hapo na kampuni ya bBioland kwa kushirikiana na wananchi, mwalimu mkuu wa shule hiyo, James Mwalukasa, amesema shule yake inakabiliwa na tatizo kubwa la upungufu wa miundombinu hasa vyumba vya madarasa na nyumba za walimu, ambapo zaidi ya wanafunzi 850 wanaosoma shuleni hapo wamekuwa wakitumia vyumba vinne vya madarasa kabla ya kujengewa vyumba hivyo vitatu ambavyo vimezinduliwa.
 
Akikabidhi vyumba hivyo vya madarasa kwa naibu spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania, dk. Tulia akson mwansasu, meneja wa kampuni ya Bioland, Felix Mtawa amesema wameamua kushirikiana na wananchi kujenga vyumba vya madarasa katika wilaya za Kyela na Rungwe kwa kuwa wanatambua elimu ndio kila kitu kwenye jamii.
 
Mbunge wa Busokelo, Atupele Fred Mwakibete amesema kampuni ya Bioland imekuwa na msaada mkubwa katika kusaidia kutatua changamoto za elimu ambapo wameahidi kujenga zaidi ya vyumba vya madarasa 1700 ifikapo mwaka 2020, huku Naibu Spika,Dkt.Tulia Akson Mwansasu akiwataka wananchi kushirikiana na wadau hao kuhakikisha watoto wao wanasoma wakiwa katika mazuri.
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Kuelekea uchumi wa viwanda. Je mfumo wa elimu umebadilika kujibu mahitaji ya nchi
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather