Independent Television Ltd
Jeshi la polisi kanda maalum ya DSM latangaza operesheni maalum ya kuwabaini wezi wa vifaa vya magari.

Jeshi la polisi kanda maalum ya dar es salaam limetangaza operesheni maalum ya kuwabaini wezi wa vifaa vya magari ambapo wafanyabiashara wote ambao wanauza vipuri vya magari vilivyotumika wanatakiwa kuonyesha nyaraka za kuingiza bidhaa zao hapa nchini pamoja na risiti za kodi walizolipia kodi na kama watashindwa kufanya hivyo wataunganishwa na kundi na wezi wa vifaa vya magari.

Operesheni hiyo imetangazwa na kaimu kamanda wa polisi wa kanda hiyo Lucas Mkondya wakati akitangaza operesheni hiyo kwa umma ambapo amesema maduka mengi ya vifaa vya magari vimekuwa vikitumika kama sehemu ya kuuzia vitu vya wizi.
Aidha kamanda huyo amesema watahakikisha wanakomesha mtandao wote wa wezi wa magari na tayari wametuma kikosi maalaum cha polisi nje ya nchi kwenda kubaini mtandao huo wawezi wa magari.
 
Baadhi ya wananchi  wamepongeza mpango wa kuwabana wezi wa vifaa vya magari kwani wizi huo umekuwa sugu na watu wamekuwa wakiishi bila ya kuwa amani na magari yao.
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Utaratibu wa viongozi kukutana na wananchi kusikiliza kero zao. Je, utasaidia kuongeza uwajibikaji kwa watendaji serikalini?
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather