Independent Television Ltd
Wakulima wa Korosho wamwomba Rais Magufuli kuangalia mwenendo wa utoaji ruzuku wilayani Mkuranga.

Wakulima wa zao la Korosho wilayani Mkuranga mkoani Pwani wamemuomba Rais John Pombe Magufuli kuingilia kati mwenendo wa utoaji ruzuku za pembejeo ya Salpha inayotolewa na serikali kwavile baadhi ya vijiji kila mkulima anapewa mfuko mmoja wa Salpha tofauti na mahitaji halisi.

Wakizungumza katika mkutano wao uliowashirikisha viongozi wa vijiji,vitongoji, wakulima wa kata ya Dondo na Kisiju kuzungumzia changamoto za usambazaji wa  pembejeo kuelekea msimu wa Korosho wakulima hao wamesema utaratibu uliowekwa umegubikwa na urasimu huku baadhi ya wakulima wakiwatupia lawama viongozi wa vijiji kushindwa kutatua kero ya wanyama waharibifu wakiwemo Kima wanaoharibu mazao yao.
 
Kwa upande wake mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilayani Mkuranga  Bw.Hamisi Mtitu akizungumza na wakulima hao amewaonya baadhi ya watendaji wanaojiorodhesha majina yao maradufu katika kila kijiji kwa lengo la kujipatia pembejeo ya Salpha kisha kuwauzia wakulima kinyume na utaratibu uliowekwa na serikali.
 
Awali akitoa ufafanuzi juu ya ugawaji wa ruzuku ya pembejeo ya Salpha inayolalamikiwa na wakulima wengi wa zao hilo afisa kilimo kata ya Kisiju Yahaya Mfikirwa Chomboko licha ya kuwahimiza wakulima kufanyia palizi mashamba yao amekiri uwepo wa upungufu wa pembejeo ukilinganisha na mahitaji halisi ya wakulima huku diwani wa kata ya Kisiju akijibu changamoto ya wanyamawaharibifu kwa wakulima hao.
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Wakulima kulazimishwa kuuza korosho kinyume na bei elekezi. Je ni utawala bora?
Ndio
Hapana
Vote Now
Results
Weather