Independent Television Ltd
Taasisi ya moyo ya jakaya kikwete yapata msaada wa vifaa vya upasuaji wa moyo toka Kuwait.

Serikali ya Kuwait imetoa msaada ya kifaa maalum cha kusaidia operesheni ya moyo pamoja na kitanda Vyenye thamani ya zaidi ya dola za kimarekani laki mbili ambazo ni ni zidi ya shilingi milioni 400 kwa taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete baada ya kumtambua mchango mkubwa wa taasisi hiyo katika matibabu ya Moyo ndani ya nje ya nchi.

Akizungumza kabla ya kupokea vifaa hivyo, waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema toka mwaka 2015 hadi 2017 jumla ya wagonjwa 713 kati yao asilimia 61 ni watoto na Watu wazima asilimia 39 wameweza kufanyiwa upasuaji katika taasisi hiyo.
 
Balozi wa Kuwait nchini Jasem Al Najema ameipongeza taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete kwa kazi kubwa Inayofanya ya kufanya upasuaji wa moyo kwa wagonjwa toka ndani ya nje ya nchi na kuahidi kuendelea Kuisaidia ili kuweza kufikia malengo iliyojiwekea katika utoaji wa matibabu kwa kuhakikisha hakuna Watanzania wanaopelekwa nje kwa ajili ya matibabu ya moyo.
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Utaratibu wa viongozi kukutana na wananchi kusikiliza kero zao. Je, utasaidia kuongeza uwajibikaji kwa watendaji serikalini?
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather