Independent Television Ltd
Nchi ya Mauritius yaonyesha nia na utayari wa kuwekeza kwenye uzalishaji wa Sukari.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Mauritius nchini Tanzania Mhe. Jean Pierre Jhumun mwenye makazi yake mjini Maputo,Msumbiji aliyeongozana na Wawekezaji wa Uzalishaji Sukari ambao wameonyesha nia na utayari wa kuwekeza nchini.

Mbali ya ujumbe kutoka Mauritius, wengine waliohudhuria mazungumzo hayo ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Profesa Godius Kahyarara naMkurugenzi  Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF , Bw .William  Erio .
 
Katika mazungumzo hayo  Makamu wa Rais amewahakikishia wawekezaji hao ushirikiano wa Serikali na kuwaeleza kuwa Tanzania ina mazingira bora ya uwekezaji.
 
Mbali ya fursa ya uwekezaji katika Sukari, Makamu wa Rais aliainisha maeneo mengine ya kuwekeza kama vile viwanda na TEHAMA.
 
Aidha alisema pindi uwekezaji huo ukifanikiwa , Tanzania itafaidika na soko la nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na masoko mengine duniani kwa ujumla.
 
Uwekezaji huu utakuwa wa Ubia kati mashirika ya hifadhi ya mifuko ya jamii na pia kampuni nyingine za wazawa.
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto