Independent Television Ltd
Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo amekanusha taarifa za kuwepo kwa mchele na Mayai ya Plastiki nchini zinazoenea mitandaoni.
Baada ya kuenea kwa taarifa za kuwapo mchele wa Plastiki na Mayai ya Plastiki kupitia mitandao ya kijamii, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Hiiti Sillo amekanusha na kuitoa hofu jamii na kusema kwamba hakuna Mchele wala Mayai ya Plastiki nchini hivyo wasiogope kutumia kwani wamekagua vyakutosha.
 
Ametoa kauli hiyo akizungumza na ITV ambapo amesema kwamba baada ya kuona taarifa hizo walifanya uchunguzi na kujiridhisha kwamba mchele wa plastiki na mayai ya plastiki hakuna, huku akisema kwamba mchele wowote ukiwekwa kwenye maji ikiwa ni waplastiki utaelea lakini kama sio wa Plastiki hauwezi kuelea,ambapo amewataka pia wananchi wawapo na wasiwasi wa jambo fulani nivema kufika kuwaona ili kama kuna jambo lenye kuleta wasiwasi wakalifanyia kazi kuliko kutumia mitandao ya kijamii kusambaza taarifa ambazo hazina ukweli na kutia hofu jamii.
 
Bwana Sillo amesema mchele uliopo katika soko hivi sasa ambao wao kama mamlaka wanaufahamu unatokana na zao la mpunga, hivyo katika uchunguzi waliofanya kwa kipindi chote baada ya uvumi huo hakuna eneo walilobaini kama kuna mchele ambao umetokana na Plastiki, amesema kwenye mchele kuna wanga hivyo mchele ukiwa haujakaa mda mrefu ukiupika vizuri ukaufinyanga unaweza ukadunda na hiyo huenda ndio ilizusha hofu.
 
Hata hivyo Mkurugenzi huyo ameongeza kwa kusema kwamba kwa wanaotumia mitandao ya kijamii kusambaza taarifa ambazo hazina ukweli wajiepushe kwani serikali ina mkono mrefu wa kuwabaini hivyo tayari wamekwisha wasiliana na mamlaka ya mawasiliano nchi (TCRA) na vyombo vingine kusudi kukamata wanaosambaza taarifa hizo na kujua nini dhamira yao kuu haswa.
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Utaratibu wa viongozi kukutana na wananchi kusikiliza kero zao. Je, utasaidia kuongeza uwajibikaji kwa watendaji serikalini?
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather