Independent Television Ltd
Kiwanda cha kuzalisha sukari kujengwa wilayani Chamwino.

Halmashauri ya wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma imesaini mkataba wa awali wa makubaliano ya ujenzi wa kiwanda cha sukari na mwekezaji kutoka kampuni ya Purandare Industries Limited ya India katika kijiji cha Dabalo chenye wakulima zaidi ya 200 wenye mashamba ya  miwa yanayofikia hekari 1167. 

Wakizungumza katika zoezi la kusaini makubaliano hayo mkurugenzi wa wilaya ya Chamwino Athumani Masasi na mkurugenzi wa kampuni ya Purandare Stalish Purandare wamesema kiwanda hicho kitaongeza pato la halmashauri, kitatoa ajira na kuongeza thamani ya zao la miwa pamoja na kuboresha maisha ya wakazi wa maeneo hayo.
 
Kwa upande wake mkurugenzi wa maendeleo na mipango kutoka bodi ya sukari Tanzania, Abdul Mwakemwa amesema mradi huo ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa taifa wa maendeleo ya sukari.
 
Naye mkuu wa wilaya ya Chamwino Vumilia Nyamogha anasema  hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la rais John Magufuli kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda na kuwataka wananchi wa Chamiwno kuchangamkia fursa .
 
Kiwanda hicho kitakapokamilika kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 15,000 za sukari kwa mwaka na kitatoa ajira kwa watanzania wasiopungua 2,000 na pia kitaongeza idadi ya wakulima watakaozalisha miwa hadikufikia wakulima 3,000.
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Utaratibu wa viongozi kukutana na wananchi kusikiliza kero zao. Je, utasaidia kuongeza uwajibikaji kwa watendaji serikalini?
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather