Independent Television Ltd
Mkuu wa wilaya Kilombero apiga marufuku sherehe kufanyika bila kibali cha mtendaji wa eneo.

Mkuu wa wilaya ya Kilombero Bw, James Ihunyo amepiga marufuku kwa mtu yeyote kufanya sherehe bila kibali kutoka kwa mtendaji wa eneo husika ikiwa ni pamoja na kuuza chakula kiholela jambo litakalo saidia mavuno yaliyo patikana msimu huu kutumika kwa uangalifu na kujikinga na athari za njaa zinazo weza kujitokeza kwa msimu ujao.

Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani la mji wa Ifakara Ihunyo amesema serikali yake ya wilaya imejipanga kuhakikisha sherehe zisizo za lazima hazifanyiki nakuwataka watendaji na madiwani kushirikiana kukemea vitendo hivyo.
 
Diwani wa kata ya Viwanja Stini ambaya ni Mwenyekiti wa halimashauri ya mji wa Ifakara Benard Mbilinyi amesema licha ya halimashauri hiyo kujitahidi kukusanya mapato lakini bado zipo changamoto mbalimbali ikiwa kucheleweshwa kwa fedha kutoka serikali kuu.
 
Awali kabla ya kikao hicho kuanza Mbunge viti maalum mkoa wa Morogoro kupitia chama cha Mapinduzi CCM mchungaji Getruda Lwakatare aliapishwa kuwa mjumbe kamili wa baraza hilo la madiwani.
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Utaratibu wa viongozi kukutana na wananchi kusikiliza kero zao. Je, utasaidia kuongeza uwajibikaji kwa watendaji serikalini?
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather