Independent Television Ltd
TCU yawataka wazazi wanaopeleka watoto wao kusoma nje kuhakikisha wanapata uthibitisho katika tume hiyo.
Tume ya vyuo vikuu nchini tcu imewataka wazazi wanaopeleka watoto wao kusoma nje ya nchi kupitia mawakala mbalimbali kuhakikisha wanapata uthibitisho kutoka katika tume hiyo ili kuepuka utapeli na pia kujiridhisha kama vigezo na masharti vimezingatiwa.
 
Afisa uhusiano wa tume hiyo Bwana Edward Mkaku ametoa tahadhari hiyo jijini Dar es Salaam ambapo amesema ni nyema wazazi na walezi wenye lengo la kupeleka wanafunzi kusoma nje ya nchi kujihakikishia wanavibali kutoka tcu kwa lengo la kujiepusha na mawakala wasio waaminifu lakini pia kuwa na uhakika wa programu na chuo atakachoenda kusoma mwanafunzi.
 
Moja wa mawakala wanaojishuhulisha na usajili wa wanafunzi wanaoenda kusoma nje ya nchi Bwana Abdulimaliki Molel mesema kwa sasa ni vyema serikali ikaweka utaratibu wa kusajili na kufuatilia mawakala ili kupunguza mawakala wasio na sifa stahiki.
 
Mwenyekiti wa umoja wa wazazi na walezi wa watoto wanaosoma nje ya nchi wameendelea kuiomba serikali kupitia tcu kuhahikisha wanaweka sheria kali kwa mawakala wasio na sifa kuwa wamekuwa wakidanga wazazi hatua ambayo inawasababishia hasara kubwa na kupotezea wanafunzi muda.
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Utaratibu wa viongozi kukutana na wananchi kusikiliza kero zao. Je, utasaidia kuongeza uwajibikaji kwa watendaji serikalini?
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather