Independent Television Ltd
EWURA kuendesha operesheni kuwabaini wanaouza mafuta yanayopatikana kwa njia zisizo halali.

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma ya Nishati na Maji (EWURA) inatarajia kuendesha operesheni maalumu katika mikoa ya Kanda ya ziwa na Kanda ya Kaskazini ya kuvikagua vituo vya mafuta ili iweze kuwabaini baadhi ya wamiliki wa vituo hivyo wanaouza mafuta kwa bei ya chini ambayo inadaiwa wanayapata kwa njia zisizo halali jambo ambalo linawapa changamoto wamiliki wengine wa vituo vya mafuta ambao hupata mafuta wa njia halali na kuyauza kulingana na bei elekezi.

Hayo yameelezwa na Mhandisi Godwin Samwel Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ewura aliyeko mkoani Kagera, akizungumza amesema mamlaka hiyo itachukulia hatua kali mmiliki yoyote wa kituo vya mafuta atakayekutwa anauzwa mafuta atakayokuwa ameyapata kwa njia zisizo halali. 
 
Awali,baadhi wamiliki wa vituo mafuta waliohudhulia semina ya siku moja iliyoandaliwa na EWURA iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mkuu wa mkoa wa Kagera wamewalalamikia baadhi wamiliki wa vituo wanaouza mafuta kwa bei ya chini hivyo wakaomba waelezwe wamiliki hao wanakopata mafuta hayo,naye Meneja mawasiliano na mahusiano wa EWURA,Titus Kaguo akizungumza amewahimiza wamiliki wa vituo vya mafuta waendeshe biashara kwa ushindani ili waweze kutoa huduma bora kwa wateja. 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Utaratibu wa viongozi kukutana na wananchi kusikiliza kero zao. Je, utasaidia kuongeza uwajibikaji kwa watendaji serikalini?
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather