Independent Television Ltd
Tanzania yatajwa kuwa miongoni mwa nchi zenye ongezeko kubwa la watu wenye matatizo ya afya ya akili.

Tanzania inatajwa kuwa miongoni mwa nchi zenye ongezeko kubwa la watu wenye ugonjwa wa akili ambao wataalamu wa afya ya akili wanasema unarudisha kwa kasi ari na ufanisi wa utendaji kazi na uzalishaji katika maeneo mengi ya kazi.

Akitoa tathmini ya matatizo ya akili nchini wakati wa Maadhimisho ya siku ya afya ya akili duniani iliyoadhimishwa kitaifa mkoani Arusha,Katibu wa Chama cha wataalamu wa afya ya akili nchini Tanzania MEHATA bi.Tasiana  Njau anasema iwapo hali hiyo haitadhibitiwa mapema itaathiri kufanikisha azma ya serikali ya kufikia kwenye uchumi wa kati.
 
Joyce Felix ni Mratibu wa afya ya akili mkoa wa Arusha anasema katika mkoa huo katika kipindi cha miaka mitatu kuna wagonjwa zaidi ya elfu sitini waliopatiwa matibabu changamoto kubwa ikiwa ni uhaba wa wataalamu wa tiba hiyo.
 
Akizungumza katika Maadhinisho hayo Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa wa Arusha  Edna Munisi anasema serikali utaendelea kushirikiana na wataalamu wa ndani na nje kutoa tiba ya magonjwa hayo na hapa anatoa angalizo kwa waajiri kuepuka kuwanyanyapaa watumishi wenye matatizo ya afya ya akili.
 
 
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Utaratibu wa viongozi kukutana na wananchi kusikiliza kero zao. Je, utasaidia kuongeza uwajibikaji kwa watendaji serikalini?
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather