Independent Television Ltd
LHRC yampongeza Rais Magufuli kwa kuweka wazi msimamo wake wa kutokuunga mkono adhabu ya kifo.

Kituo cha Sheria na Haki za binadanu kimempongeza Rais John Pombe Magufuli kwa kuweka wazi msimamo wake wa kutokuunga mkono adhabu ya kifo na kumuomba atoe maelekezo ili sheria ya kifo ibadilishwe na isiwepo nchini huku wakieleza madhara yake.

Tamko hilo limetolewa jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi wa kituo hicho Bi Anna Henga ikiwa ni siku moja kabla ya maadhimisho ya siku ya kupinga adhabu ya kifo duniani ambapo amesema adhabu hiyo ni ya kikatili isiyo ya staha,inayotweza utu wa binadamu na inafanya serikali ionekane kama mhalifu wa kuua.
 
Baadhi ya wananchi walitoa maoni yao juu ya suala hilo katika mahojiano maalum na ITV mbali na kueleza kufurahishwa na kauli ya rais wamesema changamoto za kiupelelezi na waendesha mashitaka zinaweza kusababisha mtu kuhukumiwa adhabu hiyo kimakosa.
 
Kwa mujibu wa ripoti ya haki za binadamu Tanzania ya mwaka 2016 takwimu zinaonyesha mwaka 2015 watu 472 waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa kati yao 452 ni wanaume na 20 ni wanawake kati ya hao wanaosubiri kunyongwa ni 228 na wengine 244 wanasubiria maamuzi ya rufaa zao ambapo licha ya adhabu hiyo kutokutekelezwa nchini tangu mwaka 1994 mahakama imeendelea kutoa hukumu hiyo.
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Utaratibu wa viongozi kukutana na wananchi kusikiliza kero zao. Je, utasaidia kuongeza uwajibikaji kwa watendaji serikalini?
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather