Independent Television Ltd
Watu 18 mbaroni kwa tuhuma za mauaji ya mtu mmoja kwa kutumia mishale yenye sumu.

Jeshi la polisi Kanda Maalum ya Tarime na Rorya mkoani Mara, linawashikilia watu 18 kwa tuhuma za mauaji baada ya kumshambulia kisha kumchoma mishale yenye sumu mkazi mmoja wa kitongoji cha Mwara bw.Magige Mesenda na kusababisha kifo chake.

Kamanda wa polisi wa kanda maalum ya tarime na rorya kamishina msaidizi,Mwandamizi SACP Henry Mwaibambe,amesema kuwa kikundi hicho kimekuwa kikijihusisha na mauaji ya watu mbalimbali kimekamatwa kikiwa na silaha za jadi ambazo zimekuwa zikitumika kufanya vitendo hivyo vya mauaji.
 
 
Comments
Be the first to comment
ITV SHOWS
Kipima Joto
Utaratibu wa viongozi kukutana na wananchi kusikiliza kero zao. Je, utasaidia kuongeza uwajibikaji kwa watendaji serikalini?
Ndio
Hapana
Sijui
Vote Now
Results
Weather